Mtoto wa Trump azidi kuandamwa Marekani

NEW YORK-
MTAYARISHAJI wa mkutano baina ya wakili wa Urusi, na Donald Trump Junior, Rob
Goldstone ameeleza kuwa mtoto huyo wa kiume wa Rais Donald Trump, alielewa dhumuni
la mkutano huo.
Hayo yanajiri
muda mfupi, baada ya Trump Junior kuvifokea vyombo vya habari kwa madai ya
kupotosha kile alichokizungumza juzi na kudai kuwa hakuwa akifahamu lolote kuhusu
mkutano huo.
Kwa mujibu
wa barua pepe ambayo gazeti la New York Times iliipata kutoka kwa Goldstone,
Trump Junior alifahamishwa vema kuwa mkutano huo utahusu barua pepe za Hilary
Clinton na si kama anavyodai yeye.
Gazeti hilo
limeripoti kuwa, watatu hao walikutana huku wakifahamu kila kitu na barua pepe
hiyo ya Goldstone ilibainisha kuwa Serikali ya Urusi ndiyo chanzo kikuu cha
kuvuja kwa barua pepe za Clinton.
Lakini,
gazeti hilo limeandika kuwa hakukuwa na maelezo yoyote yale kuhusu namna gani
Urusi iliingilia uchaguzi huo wa mwaka jana na kumsaidia Trump kuingia
madarakani.
No comments