Mwanaume atekwa na kubakwa na wanawake watatu Zimbabwe
Kijiji cha Makoni
HARARE- MWANAUME mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka
39, amelazwa katika hospitali ya Waza jijini hapa, baada ya kuvamiwa na
kutekwa, kunyweshwa dawa za kulevya, kabla ya kufanyishwa mapenzi bila ridhaa
yake na kisha kutupwa pembezoni mwa barabara kuu.
Inadaiwa
kuwa tukio hilo limetekelezwa na kundi la wanawake, ambalo limekuwa
likijihusisha na utekaji na ubakaji wa wanaume na kwenda kuwafanyisha mapenzi
na kukusanya manii yao.
Madaktari wa
hospitali ya Waza ambako mwanaume huyo ambaye anadaiwa kutoka kijiji cha
Makoni, wilayani Chitungwiza amelazwa kwa ajili ya matibabu, wamethibitisha
kuwa mwanaume huyo amefanyiwa ukatili wa kijinsia na wanawake hao.
Mara baada
ya kuzinduka na kupata uwezo wa kuzungumza, mwanaume huyo amewaambia maofisa wa
polisi kwamba alivamiwa na wanawake hao ambao walikuwa wakitumia gari aina ya
BMW la bluu lenye namba za usajili za Afrika Kusini.
“Walikuwepo
wanawake watatu kwenye gari hilo wakati nilipoambiwa nipande wakati nilipokuwa
nikisubiri basi kituoni mnamo Julai 2, mwaka huu. Mara baada ya kupanda,
nilipewa kinywaji na baada ya kunywa nilianza kujisikia kizunguzungu,”
“Baada ya
hapo niliamka siku nyingine, nikajikuta nikiwa kwenye chumba kidogo chenye giza
totoro. Nililazimika kujikagua na ndipo nilipojikuta nikiwa sina fedha kiasi
cha dola za Marekani 120 (sh 264,000) nilizokuwa nazo na pia nilikuwa na
michubuko kwenye kiungo change cha uzazi” anasema mwanaume huyo.
Baada ya
kujikagua na kubaini kuwa na michubuko hiyo, mwanaume huyo alisema punde si
punde wanawake hao walikuja tena chumbani hapo na kumtaka afanye nao mapenzi.
Anaeleza kwamba
baada ya kutakiwa kufanya nao mapenzi, aliwakatalia na ndipo mmoja wa wanawake
hao alitoa bastola na kumnyooshea huku akitishia kumpiga risasi na kumuua huku
akimfunga mikono.
Mara baada
ya kufungwa mikono, wanawake hao walitoa kinywaji kimoja na kumlazimisha mwanaume
huyo anywe na kisha mmoja wao akaanza kuvua nguo na kumlazimisha mwanaume huyo
afanye naye mapenzi.
“Baada ya
kulazimishwa kunywa kile kinywaji, mwanamke wa kwanza alivua nguo zake na
kunilazimisha kufanya naye mapenzi. Baada ya hapo mwingine naye alinibaka bila
kutumia kinga, licha ya wenzake kumuomba asifanye hivyo bila kinga,” mwanaume
huyo amewaambia polisi.
Mnamo Julai
4 mwaka huu, wanawake hao walimvisha mateka wao kinyago cha kufunika uso na
kisha kumlazimisha kuingia kwenye gari na kwenda kumtupa kando kando ya
barabara kwenye kijiji cha Muruta.
Baada ya
kutupwa kando kando wa barabara, mpita njia mmoja alimuona mwanaume huyo na
kisha kutoa taarifa polisi ambao nao walifika eneo hilo na kumkimbiza
hospitalini.
tukio hilo
la kutekwa na kubakwa kwa wanaume nchini, linaelezwa kuwa si la kwanza kutekelzwa
na genge la wanawake hao wanaodaiwa kusaka manii ya wanaume.
Wanawake hao
wamekuwa wakitekeleza utekaji huo na kisha kuwafanyisha mapenzi wanaume pasina
ridhaa zao na kisha kukusanya manii ambazo huziuza kwa wahitaji ambao
hawafahamu kuwa zimekusanywa kwa njia zisizo halali.
Polisi wanaendelea
na uchunguzi ili kuwabaini wanawake hao na wameitaka jamii iwe macho, kwani
matukio hayo yamekithiri.
Mail Online
No comments