Header Ads

Nitamtwanga Mayweather raundi nne za awali- McGregor



McGregor na Mayweather wakitambiana

LOS ANGELES- BONDIA Conor McGregor ameahidi kumtwanga mpinzani wake, Floyd Mayweather ndani ya raundi nne za awali watakapokutana mnamo Agosti 26, mwaka huu.
McGregor alisema hayo wakati wawili hao walipokutana kwa ajili ya kulizungumzia pambano lao la Agosti 26. Wametokea mbele ya maelfu yamashabiki wao katika mkutano na waandishi wa habari mjini Los Angeles.
“Upinzani atakaoupata kutoka kwangu hajawahi kuupata kamwe, nitamtwanga ndani ya raundi nne za mwanzo tu” alisema McGregor, 28.
Baada ya tambo za McGregor, Mayweather alimjibu kwamba; “Nakuhakikishia nitaharibu uso wako.” Mpambano huo unatajwa kuwa miongoni mwa itakayovutia zaidi duniani.

No comments

Powered by Blogger.