Lunch Time; Keita alike jezi ya Liverpool # Morata ndani Madrid # Ozil ataka £350,000 mkataba mpya Arsenal
LONDON- KIUNGO anayewindwa wa timu ya RB Leipzig na Liverpool, Nabil
Keita, amedaiwa kutoa kiashiria muhimu kinachoonesha kwamba anataka kukipiga
Anfield. Keita anadaiwa ku ‘like’ picha iliyowekwa mitandaoni inayomuonesha
akiwa na jezi nyekundu ya Liverpool. Liverpool Echo.
Windo la Chelsea, Alvaro Morata, anadaiwa kuwepo kwenye orodha ya
wachezaji wa Real Madrid ambao wanaenda kwenye ziara Marekani. Morata (24)
anatarajiwa kuwaonesha Man United makali yake watakapokutana hivi karibuni
mjini Los Angeles. ESPN.

Mesut Ozil amedai kuwa anataka kubaki Arsenal na anategemea kutia saini
mkataba mpya na washika bunduki hao wa London. Mjerumani huyo amebakiza mwaka
mmoja kwenye wake na anataka alipwe pauni 350,000 (sh bilioni 1.02) kwa wiki. Daily
Mail.

Kampuni za kuchezesha Kamari, zimeripotiwa kupunguza dau lao waliloweka
kuhusu uwezekano wa Alexis Sanchez kujiunga na Ma City. Mchezaji huyo amekuwa
akihusishwa mara kwa mara kuhama klabuni hapo. Manchester Evening News.

Dau la Man City kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa pembeni wa Tottenham
Hotspurs, Kyle Walker, linadaiwa kuwa pungufu kwa takribani pauni milioni 10
(sh bilioni 29). Walker anadaiw akuwa na thamani ya pauni milioni 50 (sh
bilioni 145). Evening Standard.
Kocha wa West Brom Albion, Tony Pulis anadaiwa kutaka kuwasajili kwa
mkupuo wachezaji wawili wa Man United, Chris Smalling (27) na Phil Jones (25). Wachezaji
hao wamebakiza miaka miwili kila mmoja kwenye mikataba yao. Daily Mail.
Everton wanaweza wakaikosa huduma ya beki wa Uholanzi na Ajax, Jairo
Riedewald (20), ambaye tayari Ajax imeshafikia makubalini na Crystal Palace. Daily
Post.
No comments