Header Ads

China kuweka kambi ya jeshi Djibouti



Picture of Chinese naval personnel in Djibouti in 2015

DJIBOUTI CITY- MELI zinazowasafirisha wanajeshi wa China kuja nchini, kuweka kambi ya Jeshi ya China ambayo ndiyo ya kwanza ya kigeni kwa taifa hilo.
China inasema kuwa, kambi hiyo itatumiwa kwa huduma za kulinda amani na za kibinadamu Afrika na Magharibi mwa Asia.
Pia itatumiwa kwa ushirikiano wa kijeshi, mazoezi ya kijeshi na huduma za uokoaji. China imewekeza katika nchi za Kiafrika, na pia imeboresha kwa haraka jeshi lake miaka ya hivi karibuni.
Shirika la habari ya Xinhua lilisema kuwa, meli hizo ziliondoka bandari ya Zhanjiang katika mkoa wa Kusini wa Guangdong jana lakini halikutaja idadi ya wanajeshi au meli zilizoplelekwa Djibouti au ni lini kituo hicho kitaanza kutangaza huduma zake.
Xinhua lilisema kuwa kituo hicho cha Djibouti, kinabuniwa kufuatia mazungumzo kati ya nchi hizo mbili. Kituo hicho kinaonekana kama hatua ya China ya kuwa na usemi wa kijeshi eneo hilo.
BBC

No comments

Powered by Blogger.