NASA Kenya yapoteza kesi ya kusitisha uchaguzi
NAIROBI- MUUNGANO
wa upinzani nchini (NASA), umepata pigo kufuatia kupoteza kesi nyingine dhidi
ya Tume ya Huru ya Uchaguzi (IEBC).
Muungano huo
unaoongozwa na kiongozi wa upinzani na mgombea wa urais, Raila Odinga,
ulipoteza ombi ulilowasilisha mahakamani ukitaka uchaguzi kusitishwa katika
kaunti zilizoathirika ama kata iwapo mfumo wa kielektroniki wa kupiga kura
utafeli.
Katika ombi
hilo, NASA ilihoji kwamba IEBC ilifeli kuweka mfumo mahsusi kama inavyohitajika
kisheria.
Upinzani
ulitegemea kifungu cha 55 cha sheria ya uchaguzi, ambacho kinaitaka IEBC
kuahirisha uchaguzi hadi pale mfumo mahsusi wa kupigia kura utakapowekwa.
Lakini, jopo
la majaji likiongozwa na Jaji Kanyi Kimondo, pamoja na Hedwig Ong'udi na Alfred
Mabeya waliipinga kesi NASA wakisema IEBC imeweka mikakati ya kukabiliana na
tatizo la kufeli kwa mfumo huo wa upigaji kura.
Walikubaliana
na IEBC kwamba, tume hiyo imeweka mikakati ya kukabiliana na utambuzi wa wapiga
kura na urushaji moja kwa moja wa matokeo iwapo mfumo huo utafeli.
Kulingana na
majaji hao, NASA ilishindwa kuelezea kesi yao na kuongezea kwamba, ombi hilo
pia linaweza kuliweka taifa hilo katika hali ya sintofahamu.
BBC
No comments