Kombe la Mataifa Afrika sasa kufanyika Juni na Julai
RABAT- SHIRIKISHO
la Soka Afrika (CAF), limesema kuwa kombe la Mataifa Afrika (CAN) 2019,
litafanyika Juni na Julai.
Mashindano
hayo huwa unafanyika Januari na Februari, na kusababisha migogoro na vilabu vya
Ulaya ambavyo hulazimika kuwatoa wachezaji katikati ya msimu.
Kinyang'anyiro
hicho cha 2019 kitakachoandaliwa Cameroon, kitashirikisha timu 24 badala ya 16.
Mabadiliko hayo yalitiwa sahihi na kamati kuu ya CAF, katika mkutano
uliofanyika mjini hapa.
Uongezaji wa
timu hizo unaweza kusababisha matatizo kwa Cameroon ambayo itaanda fainali
ijayo, huku waziri wa michezo wa taifa hilo la Afrika ya Kati akilazimika
kukataa ripoti kwamba maandalizi yalikuwa nyuma.
Hata hivyo,
CAF imeshindwa kubadili miaka ya kufanyika na badala yake yataendelea kila
baada ya miaka miwili barani Afrika. CAF ilikuwa inapanga iwapo itaruhusu
mataifa kutoka mabara mengine kushiriki ama hata kuandaa michuano hiyo.
Tangazo hilo
linajiri kufuatia mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na Rais wa CAF, Ahmad Ahmad
kuzungumzia hali ya soka barani Afrika.
No comments