Urusi yatishia kuwafukuza wanadiplomasia 30 wa Marekani

MOSCOW- SERIKALI imesema iko tayari kuwatimua
wanadiplomasia 30 wa Marekani na kutwaa mali za taifa hilo ikiwa ni hatua ya
kujibu vikwazo ilivyowekewa na Marekani mwaka jana.
Kwa mujibu
wa baadhi ya maofisa wa Serikali, vitisho hivyo vimetolewa na Wizara ya Mambo
ya Nje ya Urusi na kunukuliwa na gazeti la kila siku la Izvesta.
Desemba
mwaka jana, utawala wa Rais Barrack Obama uliwatimua wanadiplomasia 35 wa Urusi
na kufunga makao mawili ya kijasusi. Hatua hizo ni jibu kwa madai ya kuwa,
Urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani.
Urusi tayari
iko chini ya vikwazo vya Marekani. Timu ya Rais wa sasa, Donald Trump nayo iko
chini ya uchunguzi, kufuatia madai ya Urusi kuingia kati kampeni ya mwaka
uliopita. Hata hivyo, Urusi imekana madai hayo.
BBC
No comments