Marekani na Urusi zajadiliana kuhusu majengo
Hakuna
taarifa rasmi iliyotolewa kwa Waandishi wa Habari, lakini walipoulizwa na
Wanahabari waliokuwa wakisubiri kujua hatma ya mazungumzo yao, maofisa wa Urusi
walijibu kwa kifupi kwa kusema “takriban yote yamefikiwa.”
Awali,
Urusi ilionya kuchukua hatua ya kulipiza kisasi iwapo vifaa katika majengo hayo
vinawekwa tena. Maeneo na majengo hayo, yalikuwa yakishikiliwa na Marekani
kutokana na madai kuwa yalikuwa yakitumiwa kwa shughuli za kiitelejensia
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergei Lavrov ameishutumu Marekani kwa kile
alichokiita ‘Wizi wa wazi.’
Hali
ya kisiasa nchini, imekuwa mbaya katika wakati pia uchunguzi juu ya Urusi
kuingilia kati uchaguzi wa Rais ukiendelea.
BBC
No comments