Mwanamke aliyetorokea Korea Kaskazini kuchunguzwa
Mwanamke huyo aitwaye Lim Ji-hyeon, alionekana
kwenye mitandao na televisheni za taifa hilo akisema hatua yake ya kuamua kutoroka nchini
na kurudi Korea Kaskazini ni sawa na kuitoroka ‘kuzimu ya kibepari’.
Polisi wanadai kuwa, mwanamke huyo alisafiri hapo
awali kwenda China lakini ghafla akaonekana kwenye televisheni hiyo akieleza
kuwa ameamua mwenyewe kutoroka.
Lim anadai kuwa maisha hapa nchini si sawa na
alivyokuwa akidhani hapo awali, kwani fedha ni kila kitu na kusababisha hali
kuwa ngumu iwapo mtu hana fedha.
“Si sehemu sawa na nilivyofikiria awali. Kila siku
ni sawa na kuzimu.. nilikuwa nikilia kila usiku unapoingia nikifikiria kuhusu
nchi yangu, na wazazi wangu walio Korea Kaskazini,” alisema Lim.
DW
No comments