Ajuza mzoefu wa wizi akamatwa Marekani
GEORGIA- AJUZA
mmoja anayedaiwa kuwa na miaka 86, maarufu kwa wizi wa vito tangu miaka ya 1950
ameshtakiwa tena kwa wizi.
Bibi huyo, Doris
Payne alikamatwa katika duka moja katika eneo la Chamblee mjini Georgia kwa
wizi wa vito vyenye thamani ya dola 86 (sh 189,200), kulingana na maofisa wa
polisi.
Hata hivyo,
bibi kizee huyo ameachiliwa kwa dhamana. Alikamatwa kutokana na kufungwa mguuni
kifaa maalum cha kumfuatilia mtu, baada ya kuhusika kwenye wizi katika duka
lingine.
Payne ametumikia
vifungo kadhaa kwa uhalifu aliotekeleza na anadaiwa kuiba vito vyenye thamani
ya dola milioni 2 na kusababisha kuandikwa katika makala maalum ya mwaka 2013.
Mfanyakazi
mmoja wa duka la vito, alisema bibi huyo aliiba vitu kadhaa kutoka kwa duka la
dawa, vifaa vya kielektroniki na katika duka la mboga.
Wakili wa
ajuza huyo, Drew Finding alinukuliwa na chombo kimoja cha habari akisema; “Hiki
ni kisa cha kipekee ikilinganishwa na visa vingine vilivyopita.”
“Tunazungumzia
kile bibi wa miaka 86 anachotaka ili kuweza kuishi kila siku, ikiwemo chakula
na matibabu.”
Hivi
karibuni alikiri kuiba mkufu kutika duka moja huko Atlanta. Alihukumiwa kifungo
cha nyumbani na kupigwa marufuku kuingia katika maduka ya jumla katika eneo
hilo.
No comments