Header Ads

Mwanamke aitoroka familia kurudi kwa Boko Haram



Aisha Yerima mwenye umri wa miaka 25 alizungumza na Adaobi Tricia Nwaubani

BORNO- MWANAMKE mmoja ambaye alikuwa ametekwa nyara na wapiganaji wa Boko Haram, amerudi kwa wapiganaji hao kulingana na familia yake.
Aisha Yerima mwenye umri wa miaka 25 alizungumza na Adaobi Tricia Nwaubani kabla ya kurudi akisema; “Sasa nimeona kwamba vitu vyote ambavyo Boko haram walituambia havikuwa vya ukweli. Sasa nikisilikiza katika redio, nacheka.”
Alisema hayo baada ya kukamilisha mpango wa kumuondolea itikadi kali, lakini katika kipindi cha chini ya miezi mitano baadaye, ameitoroka familia yake na kurudi kwa wapiganaji hao.
Wakati alipotekwa na wapiganaji hao, alikuwa ameolewa na kamanda ambaye alimfurahisha kwa mapenzi na kumpa zawadi zenye thamani mbali na kumuimbia nyimbo za mapenzi za Kiarabu.
Mwanasaikolojia Fatima Akila, ambaye amefanya kazi na mamia ya wanawake waliookolewa, anasema mara nyingine wanaonyesha kuwa na uwezo mkubwa.
“Hawa ni wanawake ambao kwa kipindi kirefu hawakuwa wakifanya kazi, hawakuwa na uwezo, hawakuwa na sauti katika jamii na mara moja wakaanza kuwasimamia kati ya wanawake 30 jadi 100 ambao walikuwa chini ya udhibiti wao,” alisema Akila. 
BBC

No comments

Powered by Blogger.