Wanasayansi New Zealand wagundua chanjo ya kisonono

WELLINGTON- WANASAYANSI
nchini, wameonesha kwa mara ya kwanza kwamba chanjo maalum inaweza kutoa kinga
dhidi ya ugonjwa wa kisonono.
Hayo yanajiri
isiku chache, baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO), kuonya kwamba ugonjwa huo
wa kuambukiza kwa njia ya zinaa, umekuwa sugu dhidi ya dawa zake.
Watafiti
kutoka chuo kikuu cha Auckland wamegundua kuwa, maambukizi ya ugonjwa huo wa
zinaa yameshuka kwa takriban theluthi moja miongoni mwa watu ambao walipata
chanjo dhidi ya homa ya manjano.
Watafiti hao,
wamefuatilia kutoka kwa vijana milioni moja waliopata chanjo hiyo pindi
kulipotokea ugonjwa wa homa ya manjano nchini.
Kisonono
imekuwa sugu kutibika, kwa sababu kimezoea dawa za antibiotic. Mwandishi wa BBC
wa masuala ya afya, anasema utafiti huu unaonesha inawezekana kuwa na chanjo
dhidi ya ugonjwa.
BBC
No comments