Vijana sita wa Burundi watoweka Marekani
WASHINGTON
DC- VIJANA sita wa Burundi waliokuwa wakishiriki katika mashindano ya roboti
nchini, wameripotiwa kutoweka, polisi wanasema.
Vijana hao
ambao ni wavulana wanne na wasichana 2 walio kati ya umri wa miaka 16 na 18,
walipotea wakati wa mashindano hayo ya kwanza duniani yaliyofanyika jijini hapa.
Idara ya Polisi
ya Washington DC, imesema mara ya mwisho vijana hao kuonekana ilikuwa ni
Jumanne wakati wa makamilisho ya mashindano hayo.
Ripoti
zinasema kuwa vijana wawili kati yao, tayari wamevuka mpaka na kuingia Canada
lakini ripoti hiyo bado haijathibitishwa na polisi.
Jana, idara
hiyo ya polisi ilibandika picha zenye sura za vijana hao sita waliopotea katika
mtandao wao wa Twitter, wakiwataka raia kuwasiliana nao iwapo watakuwa na
habari yoyote kuwahusu.
Vijana hao
wametambulika kuwa Don Ingabire, Kevin Sambukiza, Nice Munezero, Audry
Mwamikazi, Richard Irakoze na Aristide Irambona.
Waandaaji wa
mashindano hayo, wanasema kuwa waliwaeleza polisi baada ya msimamizi wa timu
hiyo ya Burundi kushindwa kuwapata vijana hao.
Katika
taarifa hiyo, msemaji wa mashindano hayo Jose Escotto alisema, ripoti kamili
imewasilishwa kwa polisi ambao wanachunguza kisa hicho, kulingana na gazeti la
The Washington Post.
Mashindano
hayo ya siku 3, yalihudhuriwa na timu 150 zilizokuwa zikishindana. Mashindano
hayo yanalenga kuwashawishi vijana kukuza vipaji vyao katika masomo ya sayansi,
technolojia, uhandisi na hesabu.
BBC
No comments