Header Ads

Mtoto Bradley kuzikwa Ijumaa

https://www.thesun.co.uk/wp-content/uploads/2017/05/nintchdbpict000324112507.jpg?strip=all&w=960&quality=100



LONDON- UNAMKUMBUKA yule mtoto ambaye alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Saratani? Ni yule aliyekuwa shabiki mkubwa wa Sunderland ya Uingereza.
Iko hivi, mtoto huyo, Bradley Lowery ambaye alifariki wiki iliyopita, familia yake imetoa utaratibu wa maziko ya mtoto wao yatakayofanyika Ijumaa na kuwataka waombolezaji kuvaa fulana za soka ili kukumbuka miaka sita ya maisha yake.
Shabiki huyo mkubwa wa Sunderland ambaye alijenga urafiki mkubwa na mchezaji kipenzi chake, Jermain Defoe, alipoteza vita vyake na saratani adimu kwa watoto ijulikanayo kama neuroblastoma Ijumaa. 
https://www.thesun.co.uk/wp-content/uploads/2016/12/nintchdbpict000289001913.jpg?w=960&strip=all&quality=100
Habari yake iligusa nyoyo za watu duniani kote na alililiwa na mamilioni ya watu wakiwamo maarufu.
Familia hiyo jana ilitoa taarifa juu ya maziko yake ambayo yatafanyika kwenye Kanisa Katoliki la Mt Joseph mjini Blackhall Colliery, Co Durham, Ijumaa ijayo.
Waliandika kwenye ukurasa wa Facebook kwamba “saratani haina rangi” na watu wanavaa fulana za soka kwa heshima ya mtoto wao.
Familia hiyo pia ilikumbusha mashabiki wake, kwamba wanachanga fedha kwa ajili ya Wakfu wa Bradley Lowery na waombolezaji wanaweza kutoa fedha kwa ajili hiyo kupitia mkondoni.
Ujumbe huo ulisema: “Hii iko wazi kwa kila mtu ambaye atapenda kuja na kusherehekea maisha ya Bradley na kutoa heshima zao kumwonesha jinsi walivyompenda.
“Si kila mtu ataweza kuingia kanisani lakini kuna vipaza sauti nje kwa ajili ya watu kusikiliza misa na watu wanaweza kujipanga barabarani kama wataona inafaa.
“Baadaye kutakuwa na mialiko kwenye sherehe ya faragha makaburini. Familia imeomba kusiwe na vyombo vya habari isipokuwa kama wanahabari watakuwapo, si kikazi bali kutoa heshima zao.
“Unaweza kuvaa unavyotaka kwa ajili ya mazishi, lakini familia na marafiki wameamua kuja na kaulimbiu ya saratani haina rangi. Hivyo watavaa mashati ya soka bila kujali ni timu au rangi gani.
“Kutokana na umaarufu wa Bradley, wangependa maua ya familia tu na kama utapenda kuchangia hilo basi mchango uelekezwe kwenye Wakfu wa Bradley Lowery.”
Msichana wa miaka minane, Brooklyn Hutchinson, ambaye naye anapambana na saratani, alipatwa mshituko mkubwa aliposikia kifo cha Bradley. Alijenga uhusiano imara na Bradley, kwani walikuwa wakipata tiba ya kemikali pamoja.
Image result for Brooklyn a best friend of Bradley Lowery
Mara nyingi walionekana wakitembea pamoja kwenye kitengo cha saratani cha hospitali ya Royal Victoria, Newcastle.
Mama yake Brooklyne, Joanne, alieleza jinsi binti yake alivyopata pigo baada ya kusikia taarifa za kifo cha Bradley.
Aliiambia Daily Mirror: “Ilisikitisha sana. Aliniuliza, ‘inawezekanaje Bradley afe? Ana miaka sita tu’.
“Walipenda kucheza pamoja wodini na kuongozana kwenye chumba cha sanaa.
“Walikuwa sawa na jozi yoyote ya watoto wanaofurahi pamoja shuleni. Wakati mwingine wakiwa wanacheza na kucheka pamoja ungesahau matatizo waliyonayo.
“Nadhani hicho ndicho pia kilikuwa kikitokea kwao. Fikra zao zilisahau matibabu na siku zao ngumu.”
Brooklyn aligundulika na saratani ya figo Agosti, 2015 na tiba ya kemikali ilimsababishia kushindwa kutumia miguu na mikono yake kwa muda mfupi. Alilazimika hata kuondolewa figo moja.
Januari mwaka jana, alihakikishiwa kuwa tatizo limekwisha, lakini miezi sita badaye, wazazi wake wakachanganyikiwa kubaini uvimbe mwingine kwenye pafu lake la kulia.  Baada ya kuondolewa pafu lake Januari, hivi sasa anapata matibabu tena.
 

No comments

Powered by Blogger.