Mchezaji Manchester United ageukia Upadri
BELFASTI-
MIONGONI mwa watu wagumu na wakaidi wa kuishi maisha mengine nje ya soka,
wacheza mpira. Wao huwa hawaamini kama kuna maisha kwingineko baada ya kutundika
daluga zaidi ya kurudi kuwa makocha au wakurugenzi wa kiufundi au kumiliki
akademi za mpira.
Lakini,
hali ni tofauti kwa mchezaji wa zamani wa Manchester United, Philip Mulryne. Yeye amegeukia
Upadri na mwishoni mwa wiki alipata daraja hilo na kufanikiwa kusalisha misa
yake ya kwanza katika eneo alilozaliwa la Belfast, Ireland.

Padri
Mulryne, ambaye aliwahi kuripotiwa kupata malipo ya pauni 600,000 kwa mwaka
alipokuwa mwanasoka wa kulipwa, alirejea katika Parokia ya Mt Oliver Plunkett
iliyopo Lenadoon siku mbili baada ya kupewa daraja la Upadri mjini Dublin na
kusalisha misa yake ya kwanza Jumapili.
Padri
Mulryne alianza kucheza soka katika timu ya soka ya parokia yake, St Oliver
Plunkett.
Akiwa
katika timu hiyo, alionwa na wasaka vipaji wa Manchester United, akiwa na umri
wa miaka 14 na kualikwa kujaribiwa kisha alipewa mkataba wa miaka miwili.
Mwaka
1994, Padri Mulryne alipohitimu sekondari, alikwenda Manchester United na kuwa
mwanasoka wa kulipwa kwa mkataba wa miaka minne, alicheza mechi yake kwanza ya
kulipwa 1997 dhidi ya timu ya Ipswich Town.
Alicheza
mechi tano katika timu ya United kabla ya kuhamishiwa Norwich City 1999. Katika miaka sita aliyokuwa katika timu hiyo,
alicheza mechi 135.
Aliichezea
mechi ya kwanza timu ya Taifa ya Ireland Kaskazini mwaka 1997 dhidi ya Ubelgiji
na kuichezea mechi 27 na kufunga mabao matatu.
Baada
ya kuichezea kwa muda mfupi katika timu za Cardiff City na Leyton Orient, Padri
Mulryne alistaafu kucheza soka mwaka 2009 na baadaye alijiunga na Seminari ya
Diocesan ya Mt. Malachy iliyopo Belfast.
Kisha
alisomea falsafa katika Chuo Kikuu cha
Queens na Chuo cha Maryvale kilichopo Birmingham na kuhitimu kabla ya kwenda
Italia kusomea Theolojia katika Chuo Kikuu cha
Gregorian.
Alipewa
daraja la upadri Jumamosi katika Kanisa la Mt Saviour mjini Dublin na Askofu
Joseph Augustine Di Noia ambaye alimpongeza kwa kutimiza wito wake kwa kuamua
kumtumikia Mungu baada ya kuwa mwanamichezo.
Daily
Mail
No comments