Morata atua London kukamilisha dili la Chelsea
LONDON- MSHAMBULIAJI wa klabu ya Real Madrid, Alvaro Morata (24) ametua
jijini hapa muda mfupi uliopita ili kukamilisha uhamisho wake na kujiunga na
Chelsea.
Kwa mujibu wa video iliyowekwa kwenye ukurasa wa Twitter wa Kocha wa
Chelsea, Antonio Conte, mchezaji huyo amesema ameichagua Chelsea kwani ni timu
bora kwa sasa na iko chini ya meneja bora.
“Nimeichagua Chelsea kwani ni timu bora na ina ndoto za kufika mbali. Pia
inaongozwa na meneja mzuri ambaye napenda kufanya kazi chini yake,” alisema Morata.
Morata anatarajiwa kuelewana maslahi binafsi na Chelsea, baada ya timu
hiyo kukubali kutoa pauni milioni 70 (sh bilioni 203.3) kama ada ya uhamisho. Baada
ya hapo atapima afya muda wowote na kusaini mkataba.
Habari zaidi tutakujuza zikitufikia.
No comments