Jioni leo; Liverpool, Arsenal & Chelsea zamfuata Muller # Neymar kuwanunua Mbappe na Verratti # Vigogo EPL wamtaka Kruse
LONDON- GAZETI la The Sun limeripoti
kuwa klabu tatu za Uingereza, Arsenal, Liverpool na Chelsea zinapambana vikali
kuipata saini ya mshambuliaji wa Bayern Munich ambaye hatima yake iko shakani,
Thomas Muller.
Barcelona
wameeleza kuwa, endapo watamuuza mshambuliaji wao, Neymar kwa PSG, basi fedha
hizo zitatumika kuwasajili wachezaji wawili wa Monaco, Kylian Mbappe na Marco
Verratti.
Kwa mujibu
wa gazeti maarufu nchini Ujerumani la Bild, Chelsea na Liverpool zinashindana
vikali kumuwania mshambuliaji wa Werder Bremen, Max Kruse (29). Kruse alifunga
goli 15 katika mechi 23 alizocheza msimu uliopita.
Arsenal wameingilia
kati dili la usajili wa kiungo wa Everton, Ross Barkley (23), baada ya wao
kutangaza nia ya kumhitaji. Awali, Barkley alikuwa akitakiwa na Tottenham pekee
na alisema anahitaji pauni 100,000 (sh milioni 290) kwa wiki.
Klabu ya
Werder Bremen ya Ujerumani, imesema iko tayari kumchukua mshambuliaji wa
Manchester United, Anthony Martial (21) kwa mkopo wa msimu mmoja. Kicker.
Inter Milan
wameendelea kuikazia Manchester United, kuhusiana na ombi lao la kumtaka Ivan
Perisic (28). Inadaiwa kuwa Perisic amesema anataka kuhamia United, lakini
mashetani hao wekundu hawataki kulipa pauni milioni 48 (sh bilioni 139.2) kama
dau la usajili.
Mshambuliaji
wa Torino ambaye awali alihusishwa na Manchester United na Arsenal, Andrea
Belotti, yuko mbioni kuelekea AC Milan. Belotti atakutana na mmiliki wa Torino,
Urbano Cairo, kumweleza kuwa anataka kuondoka.
Habari zote na Sky Sports.
No comments