Mkwara wa China kwa Vietnam wasitisha uchimbaji gesi
HANOI- VIETNAM
imesitisha shughuli ya uchimbaji gesi katika eneo linalozozaniwa Kusini mwa bahari
ya China, kufuatia vitisho vikali kutoka China.
Taarifa za
kuaminika zimeiambia BBC kuwa, kampuni iliyokuwa ikiendesha uchimbaji huo
iliamrishwa kuondoka eneo hilo. Hayo yanajiri siku chache, baada ya kampuni ya
Respol kusema kuwa imegundua gesi nyingi.
Ripoti
zinasema kuwa wakurugenzi wa Respol, waliambiwa wiki iliyopita na Serikali kuwa
China ilikuwa imetisha kushambulia vituo vyake katika visiwa vya Spratly ikiwa
uchimbaji huo usingesitishwa.
China inadai
kuwa karibu eneo lote la Kusini mwa bahari ya China ni lake, visiwa ambavyo pia
vinavyodaiwa na mataifa mengine.
Vietnam
inaliita eneo hilo Block 136-03, na imeipa zabuni kampuni inayoitwa
Talisman-Vietnam. China nayo inaliita eneo hilo Wanan Bei-21 ikiwa imetoa
kandarasi kwa kampuni tofauti.
No comments