Asubuhi leo; Neymar kubakia Barcelona # Can haondoki Liverpool # Kiburi champonza Nasri # Wenger amfuata Carvalho
BARCELONA- MSHAMBULIAJI wa Brazil na Barcelona, Neymar
(25), amewaambia wachezaji wenzake nyota wa Barca, Lionel Messi na Luis Suarez
kwamba atabakia klabuni hapo licha ya PSG kufikia dau la usajili la pauni
milioni 196 (sh bilioni 525.5). Sport.
Bosi wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kiungo wake Emre Can (23), ambaye
amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake, haendi kokote na wala hauzwi licha
ya Juventus ya Italia kumtaka kwa udi na uvumba kwa dau la pauni milioni 31 (sh
bilioni 89.9). Liverpool Talks.
Manchester City imeshusha dau la usajili la Samir Nasri (30), kutoka
pauni milioni 21 (sh bilioni 60.9) hadi pauni milioni 10 (sh bilioni 29) baada
ya mchezaji huyo kulalamikiwa na wachezaji wenzake kwa kiburi. Times.
Usajili wa Alexis Sanchez (28) kwenda PSG, umebaki hewani, baada ya
mazungumzo kuhusu ada ya uhamisho pamoja na mshahara kukwama. Le Parisien.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, kwa sasa ameelekeza nguvu zake kwenye
mpango wa kumsajili kiungo mahiri wa Sporting Lisbon ya Ureno, William Carvalho
(25). Daily Star.
Chelsea inatarajiwa kuwasilisha mezani ofa ya kumsajili winga wa Arsenal,
Alex Oxlade-Chamberlain (23), ambaye pia anawindwa na matajiri wa Manchester,
Manchester City. Daily Express.
Everton imetoa dau la pauni milioni 40 (sh bilioni 116) pamoja na
kipengele cha ongezeko la pauni milioni 5 (sh bilioni 14.5), ili kumsajili
kiungo wa Swansea City, Gylfi Sigurdsson (27). Wales Online.
Swansea City wameruhusiwa kuzungumza na mshambuliaji wao wa zamani,
Wilfried Bony (28), baada ya kuonesha nia ya kumtaka raia huyo wa Ivory Coast
anayekipiga Manchester City. Sun.
Tottenham Hotspurs wanakaribia kumsajili kinda wa Hoffeinheim ya
Ujerumani, Jeremy Toljan (22), kwa dau ambalo bado halijawekwa wazi. Sun.
Liverpool imesema kwamba, haitaendeleza nia yake ya kumtaka beki wa
Southampton, Virgil Van Dijk (26) hadi hapo watakapoitwa na timu hiyo. Daily
Mail.
No comments