Header Ads

Trump aunga mkono mpango wa kuiwekea vikwazo kwa Urusi



Putin amekana nchi yake kuhusika kuingilia uchaguzi huo

WASHINGTON DC- IKULU ya White House imesema kuwa Rais Donald Trump, ameunga mkono makubaliano yasiyopendelea upande wowote yaliyoafikiwa katika Bunge la Congress, yanayolenga kuiwekea vikwazo Urusi.
Ofisa habari wa Ikulu ya White House, Sarah Huckabee-Sanders alisisitiza kuwa, licha ya hatua hiyo, awali white house ilipinga muswada wa uamuzi huo, japo kuwa kwa sasa inafurahia muswada wa mwisho uliopitishwa.
Bunge la Congress linataka Urusi iadhibiwe, kwa madai ya kuingilia uchaguzi wa urais uliofanyika mwaka jana nchini.
Bunge hilo, linatarajiwa kupiga kura kesho kupitisha muswada huo kuwa sheria inayoitaka ofisi ya Rais kutoingilia mwenendo wa hatua za kidplomasia dhidi ya Urusi.
Hata hivyo, White house imekuwa na kauli zinazotofautiana mara baada ya msimamo wa bunge la Congress katika vikwazo vipya dhidi ya tuhuma za Urusi.
Kupitishwa kwa sheria hiyo na bunge la congress, kutamnyima uwezo Rais Trump, kuondoa kikwazo chochote kitakachopitishwa dhidi ya Urusi. Urusi imeendelea kupinda shutuma za kuingilia uchaguzi huo.
BBC.

No comments

Powered by Blogger.