Mkanyagano uwanjani waua watu 8 Malawi

LILONGWE- WATU nane wakiwemo watoto saba na mtu mzima mmoja,
wamekufa huku wengine zaidi wamejeruhiwa kwenye mkanyagano uliotokea kwenye
uwanja wa taifa wa Bingu.
Taarifa ya
polisi, imeeleza kuwa kanyagano huo umetokea baada ya mamia ya watu kusongamana
wakati wakijaribu kugombania viti uwanjani hapo kwa ajili ya kuangalia mchezo
wa kirafiki baina ya Nyasa Big Bullets na Silver Strikers.
Rais Peter
Mutharika ametoa pole kwa wafiwa na familia zao kwa ujumla, na kuahidi kuwa
Serikali itafanya kila liwezekanalo kusaidia familia hizo.
BBC
No comments