Arsenal na Leicester kukipiga Agosti 11 # Everton yaanza ‘jeuri ya pesa’ # Leicester yanasa kiungo wa Sevilla

LONDON- CHAMA cha Soka
nchini (FA), kimerudisha nyuma mchezo wa Arsenal dhidi ya Leicester City, hadi
siku ya Ijumaa ya Agosti 11, mwaka huu.
Mchezo huo wa
ufunguzi, unatarajiwa kuchezwa majira ya 19:45 (kwa masaa ya Uingereza) huku
michezo mingine ikibaki kuwa Jumamosi.
Agosti 12, 2017 *saa
za Uingereza
Watford v Liverpool (12:30)
Brighton v Man City
(17:30)

Baada ya kupata
uhakika wa fedha zilizotokana na kumuuza Romelu Lukaku kwa Man United, timu ya
Everton imedaiwa kuanza mbio za kumsajili kiungo wa Swansea, Gylfi Sigurdsson
(27). Lakini watalazimika kulipa pauni milioni 40 (sh bilioni 116) kuipata
saini yake.
Klab ya Leicester
City imetangaza kumsajili kiungo wa Sevilla, Vicente Iborra, kwa kiwango cha ada
ambayo haijawekwa wazi.
Iborra
aliuambia mtandao wa klabu hiyo kwamba; “Ninafuraha kujiunga na Leicester City
na ninategemea kupata uzoefu mwingi kwenye ligi hii ya Premier League sanjari
na wachezaji wenzangu.”
Zote na BBC Sport
No comments