Bunge la Upinzani lavamiwa Venezuela

CARACAS-
WATU wanaokadiriwa kufikia 100 ambao wanadaiwa kuwa wafuasi 100 wa Serikali,
wamevamia Bunge linalodhibitiwa na Upinzani nchini na kuwapiga wabunge.
Mashuhusa wanadai
kuwa, makabiliano hayo yalitokea baada ya Kikao cha Bunge kuadhimisha siku ya
uhuru. Polisi waliokuwa wakilinda Bunge, walitazama wakati wavamizi waliokuwa
na fimbo walipovunja lango lakini Serikali imeapa kufanya uchunguzi.
Kwa mujibu
wa Spika wa Bunge, Julio Borges, watu 350 walifungiwa ndani ya bunge kwa saa
kadhaa, wakiwemo waandishi wa habari, wanafunzi na wageni wengine.
Borges
aliwataja wabunge watano waliojeruhuwa na kusema kuwa, baadhi walipelekwa hospitali
kwa ajili ya matibabu. Venezuela imetikiswa na maandamano yenye ghasia miezi ya
hivi karibuni, na sasa inakumbwa na matatizo ya kiuchumi.
Wizara ya Mambo
ya Nje imelaani ghasia hizo, ikizitaja kuwa dhuluma dhidi ya demokrasia
inayofurahiwa na watu wa Venezuela tangu ipate uhuru miaka 206 iliyopita
Kabla ya
wavamizi kuingia kwenye majengo ya Bunge, Makamu wa Rais, Tareck El Aissami
alionekana bungeni akiandamana na Mkuu wa Majeshi, Vladimir Padrino Lopez.
Inadaiwa kuwa
mara baada ya kuondoka, El Aissami alitoa hotuba akiwashauri wafuasi wa rais kwenda
bungeni kumuonesha rais uungwaji mkono. Umati mkubwa wa watu ulikuwa
ukiandamana nje ya majengo ya bunge kwa saa kadhaa kabla ya kuingia ndani.
BBC
No comments