Header Ads

Mjerumani wa IS akamatwa Mosul



https://ichef-1.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/A8A1/production/_96996134_islamicstate3.jpg

MOSUL- VIONGOZI wa mashtaka nchini Ujerumani, wanachunguza iwapo msichana wa miaka 16 kutoka Ujerumani ni miongoni mwa kundi la washukiwa wa Islamic State (IS) waliokamatwa mjini Mosul.
Msichana huyo, anadaiwa kukutwa akiwa kwenye handaki na raia wengine 19 wa kigeni. Maofisa wanajaribu kuthibitisha iwapo ni msichana huyo, ndiye aliyepotea katika mji wa Lulsnitz nchini Ujerumani mwaka uliopita.
Serikali imetangaza ushindi dhidi ya IS mjini hapa, ijapokuwa vita vinaendelea katika maeneo mengine ya mji huu wa zamani.
Vita hivyo ambavyo vimechukua miaka tisa, viliyaacha maeneo makubwa yakiwa yameharibiwa na kuwaua maelfu ya raia huku takriban watu 920,000 wakiachwa bila makazi.
Picha za msichana huyo aliyekamatwa na wanajeshi wa Iraq, zilichapishwa na vyombo vya habari vya eneo hilo.
Chombo cha habari cha Ujerumani kiitwacho DPA, kiliripoti kuwa kundi hilo la wageni lilikuwa likimiliki silaha na mikanda ya vilipuzi wakati walipokamatwa.
Washukiwa hao wanashirikisha raia watano wa ujerumani, watatu wa Urusi, watatu wa Uturuki na wawili wa Canada.
BBC.

No comments

Powered by Blogger.