Ndege ya makamu wa rais Afghanistan yazuiwa kutua
KABUL- NDEGE
iliyombeba Makamu wa Rais, Abdul Rashid Dostun imezuiwa kutua kwenye uwanja wa
ndege nchini, baada ya kurudi kutoka Uturuki.
Kwa mujibu
wa maofisa wa Serikali, ndege hiyo ilizuiwa kutua nabado haijulikani ni nani
aliyeizuia. Hata hivyo, watu wa karibu na Ashraf Ghani, wanaeleza kuwa ujio huo
haukupangwa na Serikali.
Dostun
aliondoka nchini kuelekea Uturuki mnamo Mei mwaka huu, huku kukiwa na madai
kwamba aliwaagiza watu wake kumteka, kumpiga na hata kumbaka mpinzani wake wa
kisiasa.
Amekana
kufanya makosa yoyote. Msemaji wake anasema kuwa alielekea Uturuki kwa ukaguzi
wa afya yake.
Atta
Mohammad Noor, ambaye ni gavana wa Kaskazini mwa mkoa wa Balkh, alikuwa
akisubiri katika uwanja wa ndege wa Mazar-e Sharrif kumpokea Jenerali Dostun juzi
usiku, kulingana na chombo cha habari cha Pajhwok.
Zaidi ya
watu 1000, waliandamana na gavana huyo kumpokea mpiganaji huyo wa zamani katika
mpaka huo ambao uko karibu na mkoa wa nyumbani wa Jowzjan.
Mashahidi
wanasema kuwa baadhi ya wafuasi wa Dostun walikuwa na mabango yaliyosema karibu
nyumbani kiongozi wetu, kulingana na chombo cha habari cha Reuters.
BBC.
No comments