Mezani kwetu leo; Rooney aondolewa kwenye orodha Man United # Rudiger atua London kukamilisha usajili # Man United kufa kupona kwa Morata
LONDON- NAHODHA wa Manchester United, Wayne Rooney,
31, ameondolewa kwenye orodha ya wachezaji wa timu hiyo wanaokwenda kwenye
ziara nchini Marekani, ili aweze kukamilisha uhamisho wake wa kurudi katika klabu
yake ya zamani ya Everton bure.
Pia, Everton imeonesha nia ya kumtaka mshambuliaji wa Arsenal na
Ufaransa, Olivier Giroud kwa ada ya pauni milioni 20 (sh bilioni 58). The
Sun

Kwa upande
wao, Man United wameripotiwa kufufua tena nia yao ya kumtaka winga raia wa
Croatia anayekipiga Inter Milan ya Italia, Ivan Perisic (28) kwa dau la pauni
milioni 48 (sh bilioni 139). Sky Italia
Pia, gazeti
la The Independent limeeleza kuwa Man
United wanatarajiwa kuweka msukumo wa mwisho kwenye mpango wao wa kumnasa mshambuliaji
wa Real Madrid, Alvaro Morata (24). Lakini inaripotiwa kuwa, Madrid wamekataa
kata kata kushusha dau lao wanalotaka la pauni milioni 72 (sh bilioni 208.8).
Daily Mirror wameripoti kuwa mlinzi wa kati wa Roma, Antonio
Rudiger (24) amewasili jijini London, kwa ajili ya kufanya vipimo na
kukamilisha usajili wake kwenda Chelsea kwa dau la pauni milioni 36 (sh bilioni
104.4).
Klabu hiyo
ya London ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza, wameripotiwa
kumtaka mlinda mlango wa PSG ya Ufaransa, Alphonse Areola (24). Daily Star.
Tottenham Hotspurs
wameripotiwa kumtaka kiungo mshambuliaji wa Everton, Ross Barkley (23) ili
kukiongezea nguvu kikosi chao lakini hawataki kulipa dau la pauni milioni 50
(sh bilioni 145) zinazotakiwa kama ada ya uhamisho. The Sun.

Liverpool
imeripotiwa kuweka mezani dau la pauni milioni 14.9 (sh bilioni 43.2), kama ada
ya uhamisho ya mlinzi kinda kutoka Olympic Lyon ya Ufaransa, Emmanuel Mammana
(21). Sport Review.
Televisheni ya
klabu ya Ajax, imeliambia Shirika la Habari la Goal.Com kwamba, windo la timu
za Manchester United na Manchester City, Kasper Dolberg (19), hataki kuondoka
klabuni hapo na kuelekea Old Trafford au Etihad.
Kocha wa
Newcastle United, Rafael Benitez, amewapa nafasi ya mwisho wachezaji wake, Tim
Krul (29), Henri Saivet (26), Siem De Jong (28) na Emmanuel Riviere (27) ili kuonesha
kiwango cha kumvutia kwenye michezo ya maandalizi ya msimu (Newcastle
Chronicle).
No comments