Afrika Kusini yaendeleza nia yake ya kujitoa ICC
CAPE TOWN- CHAMA
tawala nchini (ANC), kimeonesha kuwa bado kina mipango ya kuiondoa Afrika Kusini
kwenye uanachama na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
ICC
inatarajia kutangaza kesho iwapo Afrika Kusini ilivunja sheria kwa kushindwa
kumkamata Rais wa Sudan, Omar al Bashir (pichani), alipofanya ziara nchini mwaka 2015.
Rais Bashir
anashutumiwa kutekeleza mauaji ya kimbari wakati wa mzozo wa Darfur. Serikali ilikua
na mipango hiyo tangu miaka miwili iliyopita.
Ilikua ni
msukumo uliofanywa na baadhi ya Serikali za Afrika dhidi ya taasisi hiyo,
zikidai kuwa ICC imekua ikilionea bara la Afrika na viongozi wake.
Mahakama Kuu
nchini, yenyewe imesema Serikali imekua ikifanya mchakato huo kinyume na Katiba,
ikishindwa kulipeleka suala hilo bungeni.
Pamoja na
hayo ANC kimesema hakitarudu nyuma, wataendelea na mipango yao ya kujiondoa
ICC.
BBC
No comments