Header Ads

Kata ya Kigoma kuyapa mitaa majina ya nyota wa zaman waliocheza Mataifa ya Afrika 1980



http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2012/07/Zitto-Kabwe.jpg

KIGOMA- KATA ya Kigoma imememaliza vikao vya kupanga majina ya mitaa na imeamua kutoa mitaa 25 kwa ajili ya kupewa majina ya wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kilochoshiriki AFCON 1980. 
Wachezaji na makocha wote watapata mitaa kwenye eneo la Mji Mwema. Namshukuru Sana Diwani wa Kata ya Kigoma Ndugu, Hussein Haidary Kalyango kwa kufanikisha hili.
Nitajithidi wachezaji wote walio hai na walimu wao, wahudhurie shughuli maalumu ya kuzindua mitaa yenye majina yao.  Kata hii pia imetoa jina kwa Profesa Abdulrahman Mohamed Babu, kwa mchango wake kwenye umajumui wa Afrika na ukombozi wa Afrika. 
Kikosi cha Taifa Stars ya mwaka 1980 hiki hapa:

Athumani Mambosasa
Juma Pondamali
Taso Mutebezi
Jelah Mtagwa
Leodgar Tenga
Mohamed Kajole
Husein Ngulungu
Mtemi Ramadhan
Juma Mkambi
Omari Hussein
Mohamed Masewa
Thuweni Ally
Peter Tino
Ahmed Thabit
Charles Boniface
Salim Amiri
Adolf Richard
Zamoyoni Mogela
Martin Kikwa
George Kulagwa

Uzinduzi wa Mitaa Hii ya Mashujaa wetu utafanyika Juumamosi ya Kwanza ya Mwezi wa Tisa ambapo kutachezwa Mechi kati ya Timu ya Manispaa ya Lake Tanganyika SC na Timu ya Bukavu Dawa ya DRC.

Zitto Kabwe
Kigoma Mjini

Chanzo. Fahari Time

No comments

Powered by Blogger.