Header Ads

Mezani Asubuhi; Bale njia nyeupe Man United # Conte amtaka Barkley # Liverpool yamkomalia Keita



https://static.independent.co.uk/s3fs-public/thumbnails/image/2016/01/10/13/gareth-bale-23324.jpg
MADRID- KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema hawezi kumhakikishia mshambuliaji wake, Gareth Bale (28) ambaye anawindwa na Manchester United, kuwa atabakia msimu huu pale Santiago Bernabeu. Mirror.

http://i4.mirror.co.uk/incoming/article5363997.ece/ALTERNATES/s615/Ross-Barkley-Everton.jpg
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte, ameandaa pauni milioni 50 (sh bilioni 145) kwa ajili ya kuwasajili wachezaji wawili wa Uingereza, Ross Barkley (23) kutoka Everton na Alex Oxlade-Chamberlain (23) wa Arsenal. Sun.

http://a.espncdn.com/combiner/i/?img=/photo/2016/0816/r114399_1296x729_16-9.jpg&w=738&site=espnfc
Liverpool wako tayari kutoa ofa yao ya mwisho kwa RB Leipzig, yenye thamani ya pauni milioni 70 (sh bilioni 203) na kipengele kitakachoruhusu ongezeko ili kumnasa Naby Keita (22). Mirror.

https://metrouk2.files.wordpress.com/2017/05/686314800.jpg
Hatima ya usajili wa kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho (25) imezidi kuingia shaka, baada ya Liverpool kueleza kuwa hawatabadili msimamo wao wa kutomuuza mchezaji huyo licha ya kudaiwa kuelewana maslahi binafsi na Barcelona. ESPN.

http://www.parisfans.fr/wp-content/uploads/2015/05/Blaise-Matuidi-ame-du-PSG.jpg
Juventus imekaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa PSG, Blaise Matuidi (30) na kujiondoa kwenye mbio za kumsajili kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic (28). Independent.

https://www.thesun.co.uk/wp-content/uploads/2017/07/nintchdbpict0003274565322.jpg?strip=all&w=960&quality=100
Mwenyekiti wa AC Milan, Marco Fassone amebainisha kuwa wamefanya mazungumzo na wakala wa mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa (28) kwa ajili ya kumsajili. Sky Sports.

https://www.thesun.co.uk/wp-content/uploads/2017/05/nintchdbpict000321041525.jpg?strip=all&w=960&quality=100
Mshambuliaji wa Ufaransa na Real Madrid, Karim Benzema (29) anatarajiwa kusaini mkataba mpya na Real Madrid bila kujali kama klabu hiyo itamsajili Mfaransa mwenzake, Kylian Mbappe (18). Marca.

https://www.thesun.co.uk/wp-content/uploads/2017/02/nintchdbpict000296232831.jpg?strip=all&w=960
Mshambuliaji wa Juventus, Paulo Dybala (23) ambaye anawindwa na miamba miwili, Manchester United na Barcelona, amesema hana mpango wa kuondoka Juventus msimu huu. Talksport.

https://metrouk2.files.wordpress.com/2017/07/6329671261.jpg?w=748&h=498&crop=1
Bosi wa Inter Milan, Luciano Spalletti amesema angependa winga wa timu hiyo, Ivan Perisic (28) abakie klabuni hapo lakini hawezi kusema jambo gani litatokea siku za usoni. ESPN.





No comments

Powered by Blogger.