Header Ads

Iran yafanya jaribio la roketi ya kubeba satalaiti



The Phoenix rocket is launched

TEHRAN- IRAN imefanikiwa kuifanyia jaribio roketi ambayo ina uwezo wa kupeleka satalaiti hadi mzingo wa dunia, siku moja baada ya Marekani kuiwekea vikwazo vipya kufuatia mpango wake ya kinyuklia.
Roketi hiyo ya Phoenix, ilirushwa kutoka kituo kipya cha anga za juu kilicho Semnan, Kaskazini mwa nchi. Marekani ililaani jaribio hilo na kulitaja kuwa kitendo cha uchokozi.
Hilo ni jaribio la tano la roketi iliyoundwa nchini, tangu mwaka 2009. Televisheni ya taifa inasema kuwa roketi hiyo, itabeba satalaiti ya uzito wa kilo 250 hadi umbali wa kilometa 500 angani.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Marekani, anasema kuwa ikiwa itathibitishwa, jaribo hilo linaweza kukiuka maazimio ya Baraza la Umoja wa Mataifa.
Iran iliapa kujibu vikwazo vipya viivyotangazwa na Marekani, ambavyo vililenga makampuni 18 au watu ambao wameunga mkono programu za makombora za Iran.
Vikwazo hivyo vipya, vilitangazwa siku moja baada ya utawala wa Trump kusema kuwa Iran inatekeleza makubaliano ya mwaka 2015 ya kuachana na mpango wa kinyukia.
BBC

No comments

Powered by Blogger.