Header Ads

Bunge la Senate Marekani laridhia vikwazo Urusi, Iran na Korea Kaskazini



https://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/14A50/production/_97106548_gettyimages-810246808.jpg

WASHINGTON DC- BUNGE la Senate nchini, limepiga kura ya kuziwekea vikwazo vipya Urusi, Iran na Korea Kaskazini licha ya pingamizi kutoka Ikulu ya White House.
Bunge la Wawakilishi (Congress), liliidhinisha muswada huo mapema wiki hii kwa kura nyingi. Baada ya muswada huo kupita katika mabunge yote, sasa utapelekwa kwa Rais Donald Trump kuwekwa sahihi.
Lakini Trump anataka kuboresha uhusiano na Urusi, na anaweza kuukataa licha na uungwaji mkono uliopata. Vikwazo hivyo ni vya kuiadhibu Urusi zaidi, kufuatia hatua za kulimega eneo la Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014.
Lakini mjadala kuhusu vikwazo hivyo vipya, unafanyika huku uchunguzi kuhusu hatua za Urusi kuingilia kati uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 ukiendelea.
Trump mara nyingi amekana kuwa Urusi iliingilia uchaguzi huo kusaidia kampeni yake.
Waandishi wa masuala ya siasa, wanasema ikiwa Trump atajaribu kuukataa muswada huo basi itakuwa ishara tosha kuwa anaiunga mkono Urusi.
BBC.

No comments

Powered by Blogger.