Tetesi za leo; Hatima ya Conte shakani Chelsea # Lukaku ‘kulamba’ £250,000 Man Utd # Chelsea yawageukia James Rodriguez na Llorente
LONDON- MUSTAKABALI
wa kocha wa Chelsea, Antonio Conte uko mashakani baada ya meneja huyo
kukasirishwa na shughuli nzima ya usajili katika klabu hiyo (Daily Mirror).
Hatua ya
Manchester United kutaka kumsajili Romelu Lukaku (24), haihusiani na mkataba
ambao utamrejesha Wayne Rooney, 31, Everton (Liverpool Echo).
Chelsea bado
wanatarajiwa kujaribu kumsajili Romelu Lukaku (24), licha ya taarifa kuwa
mchezaji huyo amekubali kuhamia Manchester United kwa pauni milioni 75 kutoka
Everton (Guardian).
Mshambuliaji
wa Real Madrid, Alvaro Morata (24), ameachwa ‘kwenye mataa’ baada ya Manchester
United kumsajili Romelu Lukaku. Morata alikuwa na uhakika kuwa anahamia Old
Trafford (Independent).
Romelu
Lukaku amekubali kusaini mkataba wa muda mrefu Manchester United na mshahara wa
pauni 250,000 kwa wiki (Daily Star).
Chelsea
huenda wakakabiliwa na tatizo la mshambuliaji, baada ya Diego Costa kuanza
kuaga wachezaji wenzake kufuatia kuambiwa na Antonio Conte kuwa hayuko kwenye
mipango yake msimu ujao (Daily Telegraph).
Chelsea
wanajiandaa kutoa dau ‘kubwa’ ili kumsajili kiungo mshambuliaji wa Real Madrid,
James Rodriguez (AS). Pia, imedaiwa
kuwa Chelsea wameelekeza macho yao kwa mshambuliaji wa Swansea Fernando
Llorente (32), baada ya kushindwa kumpata kwa mkopo mwezi Januari (Evening Standard).
Barcelona
wamekasirishwa na nahodha wao wa zamani, Carles Puyol, baada ya mchezaji
anayemwakilisha Eric Garcia, 16, kuamua kuhamia Manchester City (Independent).
Everton
wanajiandaa kupanda dau jipya la pauni milioni 32 kumtaka kiungo wa Swansea,
Gylfi Sigurdsson, 27 (Daily Mail).
Kipa wa
Stoke City, Jack Butland (24), amesema anaweza ‘kufikiria’ iwapo Manchester
United watamtaka (Manchester Evening
News).
Arsenal
wanamtaka kiungo wa Eintracht Frankfurt, Aymen Barkok (19) (Spox).
Marseille
wanaongoza katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud (30),
kwa kitita cha pauni milioni 24.7, baada ya Arsenal kufanikisha usajili wa
Alexandre Lacazette (Daily Telegraph).
Arsenal
hawataki kulipa kiasi ambacho Leicester wanakitaka ili kumsajili winga Riyad
Mahrez (26), ambaye anatarajiwa kuondoka Leicester msimu huu (Daily Star).
Barcelona
wapo tayari kutoa pauni milioni 26 kumsajili beki wa Arsenal, Hector Bellerin (Sport). Pia, Arsenal
wanamfuatilia kiungo wa Monaco, Fabinho (France
Football).
Paris Saint-Germain
watamgeukia Philippe Coutinho, iwapo watashindwa kumsajili Kylian Mbappe kutoka
Monaco. PSG wapo tayari kutoa pauni milioni 70 kumchukua Coutinho (Le10sport). Timu hiyo imemwambia winga wake Hatem Ben Arfa (30), anaweza kuondoka Paris
Saint-Germain (L'Equipe).
Winga
Demarai Gray (21), anataka kuhakikishiwa namba Leicester huku Tottenham na Liverpool
zikimnyatia (Daily Mirror).
Licha ya
Guangzhou Evergrande kukataa, Barcelona watarejea na dau jingine kumtaka
Paulinho (Cadena SER).
Stoke City
wamekuwa na mazungumzo na Manchester City ya kumsajili kiungo Fabien Delph, 27
(Stoke Sentinel).
Real Madrid
wamekuwa na mazungumzo ya siri na PSG kuhusu Marco Verratti, 24 (Don Balon). Pia, Real Madrid wamekuwa na
mazungumzo mapya na Kylian Mbappe (Marca).
Real Madrid
watakuwa tayari kumruhusu Gareth Bale kuondoka kwa pauni milioni 88 (Diario Gol).
AC Milan
sasa wamemgeukia mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Pierre Emerick-Aubameyang,
28, na pia wanamtaka Nikola Kalinic (Gianluca
Di Marzio).
No comments