Mchezaji wa Ajax akutwa na tatizo la kudumu la ubongo
AMSTERDAM- SOKA
limeendelea kutikiswa na matukio ya wachezaji kuanguka na kupoteza fahamu
uwanjani, baada ya mchezaji wa Ajax, Abdelhak Mouri kuanguka na kuzimia ghafla
kabla ya kuthibitishwa kapata tatizo la kudumu la ubongo.
Katika mchezo
uliochezwa Jumamosi dhidi ya Werder Bremen ya Ujerumani, Nouri mwenye umri wa
miaka 20 alianguka kutokana na kupatwa na tatizo mapigo ya moyo kutokuwa sawa.
Taarifa ya
Ajax iliyotoka Jumatatu, ilieleza kuwa mara baada ya vipimo kufanyika,
ilibainika kuwa moyo wake unafanya kazi kama kawaida na vipimo vya ubongo
haukuonesha kuwa na tatizo.
Hata hivyo,
inadaiwa kuwa amepatwa na tatizo la kudumu la ubongo.
Taarifa hiyo
imesema kwamba; “Maombi yetu yako kwake na kila mtu hapa Ajax na duniani kote,
anamuombea (Nouri) apone. Familia yote ya wapenda soka, inafuatilia kwa ukaribu
maendeleo yake kiafya.”
BBC
No comments