Man United yaongoza timu kwa thamani kubwa kwenye soka
TIMU
inayocheza soka ya Marekani Dallas Cowboys, imetetea umaarufu wake kama timu ya
michezo iliyo na thamani ya juu kulingana na jarida la Forbes.
Manchester
United ambayo ni miongoni mwa timu zilizotajwa kuwa na thamani ya juu mwaka
2011 na 2012, imepanda juu klabu ya Barcelona na Reala Madrid kama timu yenye
thamani kubwa katika soka ikiwa na thamani ya dola bilioni 3.69.
Hatua hiyo
inaiweka United katika nafasi ya 3 kwa jumla.
Thamani ya
Dallas Cowboys iliongezeka kwa asilimia 5 hadi dola bilioni 4.2 huku klabu ya
mpira wa baseball New York Yankees ikiwa ya pili na thamani ya dola milioni
3.7.
Hata hivyo,
timu ya Los Angeles Rams ndio iliyopata faida kubwa na hivyo kupanda kutoka
timu hamsini bora hadi nafasi ya 12 baada ya thamani yake kupanda maradufu hadi
dola bilioni 2.9 kufuatia hatua yao ya kuondoka St Louis mwaka uliopita.
“Kuhama huko
pamoja na uwanja mpya kumesababisha kuongezeka kwa thamani ya timu za NFL,”
alisema Kurt Badenhausen, mhariri mkuu wa jarida la Forbes.
Timu za ligi
ya NFL zilikuwa katika nafasi ya 29 miongoni mwa timu hamsini bora isipokuwa
Cincinnati Bengals, Buffalo Bills na Detroit Lions ambazo hazikushirikishwa.
Hakuna timu
hata moja ya kuteleza barafuni, ama hata ile ya magari ya langalanga ya
Formular one iliorodheshwa.
Orodha ya
timu 10 zenye thamani ya juu duniani:
- 1. Dallas Cowboys $4.2bn (£3.26bn) American football
- 2. New York Yankees $3.7bn (£2.87bn) baseball
- 3. Manchester United $3.69bn (£2.86bn) football
- 4. Barcelona $3.64bn (£2.82bn) football
- 5. Real Madrid $3.58bn (£2.78bn) football
- 6. New England Patriots $3.4bn (£2.64bn) American football
- 7. New York Knicks $3.3bn (£2.56bn) basketball
- 8. New York Giants $3.1bn (£2.4bn) American football
·
9. San
Francisco 49ers $3bn (£2.33bn) American football
·
10. Los Angeles Lakers $3bn (£2.33bn) basketball
No comments