Jioni Njema; City wajitosa kwa Mbappe, wamnyakua Walker # Makelele ndiye aliyefanikisha dili la Bakayoko # Perisic haendi kokote
LONDON- MCHAMBUZI
mkongwe wa soka la Hispania, Graham Hunter, amesema kuwa klabu ya Manchester
City inafanya kila liwezekanalo ili kuinasa saini ya staa wa Monaco, Kylian
Mbappe, kwa dau ambalo bado halijawekwa wazi. Sky Sports.
Mkurugenzi
wa michezo wa Inter Milan, Piero Ausilio, amewakata ‘maini’ Manchester United
kwa kusema kwamba windo lao, Ivan Perisic, kamwe haliwezi likajiunga nao. Sky
Sports.
Manchester
City imekubali kutoa dau la pauni milioni 50 (sh bilioni 145), kama ada ya
uhamisho wa Kyle Walker wa Tottenham. Hata hivyo, imeelezwa kuwa dau hilo
linahusisha ziada (kipengele cha Man City kulipa zaidi). Sky Sports.
Imebainika
kuwa mchezaji wa zamani wa Chelsea, Claude Makelele, amesaidia kwa kiasi
kikubwa kukamilika kwa dili la usajili la kiungo wa Monaco, Tiemoue Bakayoko.
Sky Sports.

AC Milan
imeliweka jina la Leonardo Bonucci kwenye nafasi ya kwanza, ya orodha ya wachezaji
watakaosajiliwa muda wowote kuanzia sasa. Hilo linakuja, baada ya beki huyo
kuzozana na kocha wake Juventus, Massimiliano Allegri. Sky Sports.
Kiungo wa
Swansea, Gylfi Sigurdsson ameikosa ziara ya timu yake nchini Marekani kutokana
na kuachwa kukamilisha dili la kwenda Everton. Lakini inadaiwa kuwa dau la
pauni milioni 40 (sh bilioni 116) ambalo lilitolewa na Everton limekataliwa.
Sky Sports.
No comments