Marekani kuipa silaha Ukraine kupambana na waasi
DONETSK- MJUMBE
mpya wa Marekani nchini Ukriane, Kurt Volker amesema kuwa Marekani inatathmini
ikiwa itatuma silaha kusaidia wale wanaopigana na waasi wanoungwa mkono na
Urusi.
Volker
aliiambia BBC kuwa, kuihami serikali ya Ukraine itabadilisha msimamo wa Urusi. Alisema
hafikirii kuwa hatua hiyo itakuwa ni uchokozi.
Wiki
iliyopita Wizara ya Mashauri ya Nje ya Marekani, ilizitaka pande zote mbili
kusitisha mapigano Mashariki mwa Ukraine.
“Silaha za
kujilinda, zile ambazo zitaisaidia Ukraine kujilinda na kuharibu vifaru kwa
mafano, ambazo zitaizuia Urusi kuitisha Ukraine,” Volker aliiambia BBC.
Alisema kuwa,
mafanikio ya kuwepo amani Mashariki mwa Ukraine yanahitaji kile alichokitaja
mchakato wa mazungumzo na Urusi. Volker na mjumbe wa zamani wa Marekani kwenye
NATO, na aliteuliwa kwenye wadhifa huo mpya mwezi huu.
Umoja wa
Mataifa (UN), umesema kuwa zaidi ya watu 10,000 wameuawa tangu mzozo wa
Mashariki mwa Ukraine uanze mnamo April, 2014 mara baada ya Urusi kulimega eneo
la Crimea. Mapigano hayo yamesababisha
zaidi ya watu milioni 1.6 kuhama makwao.
No comments