Header Ads

Justin Bieber afuta matamasha yake yote



https://d1u4oo4rb13yy8.cloudfront.net/article/57684-zpzpsfhjsy-1494237521.jpg

LOS ANGELES- MWANAMUZIKI wa mtindo wa Pop, Justine Bieber amefutilia mbali safari yake ya kikazi katika miji iliyotajwa kufanyka mjini hapa bila kutoa sababau yoyote ya kufikia maamuzi hayo
Tamasha lililofutwa, litaathiri ratiba ya matamasha ambayo yangefanyika Amerika ya Kaskazini na Asia na ianelezwa wazi kwamba, gharama za kiingilio zitarejeshwa kwa mashabiki wake.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa masanii huyo, inasema Bieber anawapenda mashabiki wake na hapendi kuwakwaza na akatumia fursa hiyo kutoa shukrani zake kutokana na uhusiano mzuri ambao umekuwapo baina yake, uongozi na wasaidizi wake kwenye matamasha zaidi ya 150 katika mabara 6 tofauti.
Hatua hiyo, inakuja baada ya kutafakari kwa kina msanii huyo nyota wa pop ameamua hataimba tena kwenye matamasha yaliyosalia, Bieber mwenye miaka 23 hajatoa kauli yoyote wala kuandika chochote kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii
Mtandao wa celebrity news ulikinukuu chanzo kimoja na kuarifu kuwa, mwanamuziki huyo raia wa Canada amefutilia mbali matamasha yaliyo salia bila sababu za msingi
Mwishoni mwa wiki iliyopita, msanii huyo alipigwa picha akitembea mlimani na mjini hapa akiwa na na binti mdogo ambaye walionekana kuwa na mahusiano mazuri
Bieber alianza msururu huu wa matamasha kwa nguvu kubwa ya albamu yake ya ‘Purpose’ aliyoitoa Machi 2016, na tayari ametumbuiza matamasha zaidi ya 150 kwenye bara la Ulaya, Afrika, Amerika ya Kusini, Australia na maeneo ya bara Asia
Hatua hiyo ya Bieber, inakuja siku kadhaa baada ya msanii huyo kukatazwa kufanya matamasha nchini China sababu ya tabia mbaya kama ilivyoarifiwa na mamlaka mjini Beijing
Licha ya kusifia mapenzi waliyo nayo mashabiki kwa msanii huyo, lakini mamlaka hizo hazikuweka wazi ni tabia zipi za kukera alizozionesha msanii huyo kiasi cha kukatazwa kufanya matamasha nchini humo
Bieber tangu alipoanza muziki, amekuwa kama mwizi wa mioyo ya mashabiki wake kwa mapenzi makubwa waliyo nayo kwake na kazi zake.
BBC

No comments

Powered by Blogger.