Header Ads

Buhari kurejea Nigeria wiki mbili zijazo

Rais Muhammadu Buhari

LONDON- GAVANA wa jimbo la Imo nchini Nigeria, Rocha Okorocha amesema kuwa anatarajia Rais Muhammadu Buhari kurudi nyumbani kutoka Uingereza katika kipindi cha wiki mbili zijazo.
Gavana Okorocha alikuwa mmoja wa ujumbe uliokutana na rais huyo mwishoni mwa wiki iliyopita. Buhari amekuwa akipata matibabu nchini, kwa ugonjwa ambao haujawekwa wazi.
Kutokuwepo kwake kumezua hali ya wasiwasi nchini Nigeria, huku watu wakidai kwamba huenda amefariki. Wengine wamekuwa na wasiwasi kwamba huenda asirudi tena.
Baadaye Ikulu ilitoa picha za Buhari mwenye umri wa miaka 74, akikutana na magavana kutoka chama chake. Ni mara ya kwanza amepigwa picha mjini hapa, tangu aondoke Nigeria yapata siku 80 zilizopita.
Gavana Okorocha aliiambia BBC jana kwamba; “Nilikutana na mtu mwenye motisha na anendelea vema. Hajapoteza ucheshi wake kama anavyojulikana.
Kwa hivyo anaendelea vyema na tunafurahi kumuona, na tunadhani amefanya kitu muhimu kuwahakikishia raia wa Nigeria kuhusu afya ya rais wao.”
Awali, Okorocha alisema kwamba, Buhari alipuuzilia mbali uvumi kuhusu afya yake alipoulizwa. 
BBC

No comments

Powered by Blogger.