Bunge lapokea barua ya Lipumba kuwafuta uanachama wabunge nane wa CUF
DODOMA- BUNGE la Tanzania limepokea barua iliyowasilishwa
na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibarihimu Lipumba ambapo
ameainisha kuwafuta uanachama wabunge nane wa viti maalum na madiwani wawili.
Spika wa
Bunge, Job Ndugai amesema jukumu la kuwaondoa uanachama wabunge ni utashi wa
chama husika hivyo bado anaendelea kutafakari kuhusu suala hilo na atalitolea
uamuzi hivi karibuni.
Chanzo;
Ukurasa wa Twitter wa Bunge



No comments