Header Ads

Baba wa bibi harusi apigwa na radi harusini Canada



JP Nadeau beside his daughter on her wedding day

NEW BRUNSWICK- HAKUNA mtu anayependa kuona harusi ikiharibika, lakini baba mmoja ameshikwa na hofu kutokana na kilichotokea wakati wa harusi ya binntiye.
JP Nadeau anaripotiwa kupigwa na radi wakati akitoa hotuba huko New Brunswick, Canada.
“Wakati nilipokuwa nikimwambia mkwe wangu, ‘Una bahati sana’- ndipo kuliposikika kitu kama bomu,” alikimbia kituo kimoja cha habari nchini hapa.
Kando na jeraha alilopata kwenye kidole chake, Nadeau hakuhofu na sherehe hiyo ya harusi iliendelea. Kila mtu alishangazwa kwanza, lakini hilo halikusababisha sherehe kusitishwa.
“Ilikuwa harusi nzuri na iliyofana,” mke wake Nadeau alikiambia kituo cha CBC.
Nadeau amesema kuwa, yeye ni mtu mwenye bahati kwa sababu mwaka 2015 meli aliyokuwa akifanya kazi ilishika moto karibu na visiwa vya Falkland, lakini aliokolewa na Jeshi la Anga la Uingereza.

No comments

Powered by Blogger.