Mpinzani wa Obama 2008 akutwa na saratani ya ubongo
ARIZONA- OFISI
ya Seneta wa chama cha Republican, John McCain, imeeleza kuwa kiongozi huyo
amekutwa na saratani ya ubongo na kwa sasa anatafuta matibabu.
Matibabu
hayo, huenda yakashirikisha matumizi ya dawa ama mionzi kulingana na daktari
wake. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 80, yuko katika hali nzuri
akiendelea kupata ahueni nyumbani kwake.
Uvimbe huo
ulipatikana wakati wa upasuaji wa kuondoa damu ilioganda juu ya jicho lake la
kushoto. McCain ambaye alikuwa mwanajeshi aliyepigana vita nchini Vietnam, pia
aliwahi kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.
Seneta huyo
aliyehudumu kwa mihula sita na kuwa mgombea wa urais wa chama cha Republican
2008, alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Phoenix jimboni hapa wiki
iliyopita.
Uchunguzi wa
tishu ulibaini kwamba, uvimbe wa ubongo unaojulikana kama glioblastoma
ulisababisha damu hiyo kuganda kulingana na taarifa ya kliniki hiyo ya Mayo.
Madaktari wa
Seneta huyo, wanasema kuwa anaendelea kupona kutoka kwa upasuaji huo na afya
yake iko sawa.
Matibabu
yake yatashirikisha utumiaji wa dawa na mionzi. Glioblastoma ni uvimbe mbaya wa
ubongo, na huongezeka kutokana na umri wa mtu ukiwaathiri wanaume wengi zaidi
ya wanawake.
McCain
ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya seneti kuhusu huduma za jeshi, alikuwa
katika hali nzuri huku akiendelea kupona nyumbani na familia yake.
BBC
No comments