Header Ads

Makaburi ya watu wenye vipara yafukuliwa Msumbiji



Baadhi ya raia nchini Msumbiji wanaamini kwamba mtu mwenye kipara ana dhahabu

MAPUTO- Wakaazi wa wilaya ya kati ya Milange nchini, wamesema miili ya watu watano wenye vipara imefukuliwa katika kipindi cha miezi mitatu katika matukio yanayohusianishwa na imani za kishirikina.
Katika siku za karibuni, kumezuka imani potofu ambapo baadhi ya watu wanaamini kwamba kichwa cha mtu mwenye kipara kina dhahabu. Tukio hilo la kufukuliwa kwa makaburi hayo, limesababisha wakazi wa Milange kuiomba Serikali kuingilia kati na kuimarisha ulinzi.
Mwezi uliopita, kamanda mmoja wa polisi aitwaye, Afonso Dias, aliiambia kuwa misururu ya mauaji ya watu wenye vipara imekuwa ikisababishwa na imani hizo potofu.
Kufikia sasa wakaazi, na watumiaji wa dawa za kitamaduni pamoja na waliopigania uhuru wamekutana na maofisa wa taasisi ya kitaifa ya urithi na usaidizi wa haki (IPAJ).
Mwakilishi wa IPAJ, Antonio Gussi aliahidi kuwasilisha malalamishi yao kwa mamlaka husika, lakini pia akawataka kutokubali tamaduni hizo zilizopitwa na wakati katika siku za usoni.
BBC

No comments

Powered by Blogger.