Asubuhi Yetu; Neymar kutua PSG wiki 2 zijazo # Coutinho amba kuondoka # Bale kumpisha Mbappe Madrid # Conte amtamani Kane
PARIS- TIMU ya Paris St-Germain (PSG) inaamini kuwa
itakamilisha dili la uhamisho wa mshambuliaji wa Barcelona, Neymar (25), lenye
thamani ya pauni milioni 198 (sh bilioni 525.5) ndani ya siku 15. L’Equipe.

Kiungo mahiri wa klabu ya Liverpool, Philippe
Coutinho (25), ameuomba uongozi wa timu hiyo umruhusu kujiunga na Barcelona. Inadaiwa
tayari mchezaji huyo amekubaliana maslahi binafsi na Barcelona ili akazibe
pengo la Neymar anayeenda PSG. RAC1.
Mshambuliaji wa Real Madrid na Wales, Gareth Bale
(28) anatarajiwa kuondoka klabuni hapo ili kupisha ujio wa kinda wa Monaco,
Kylian Mbappe (18). Bale anaweza kujiunga na Man United muda wowote akiondoka
Madrid, baada ya kukataa ofay a Arsenal. Independent.
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amesema endapo
atahitaji kusajili mshambuliaji, basi hatasita kumsajili mfungaji bora wa msimu
uliopita wa EPL, Harry Kane (23). Daily Mail.
Arsenal wako mbioni kukamilisha usajili wa winga
Thomas Lemar (21) kutoka Monaco, licha ya Makamu wa Rais wa Monaco, Vadim
Vasilyev kudai mchezaji huyo hauzwi. Arsenal wametoa pauni milioni 45 (sh
bilioni 130.5). Sun.
Man United wanatarajia kuwa, ofa yao ya
pauni milioni 40 (sh bilioni 126) itawashawishi Chelsea kuwauzia kiungo wao,
Nemanja Matic (28) ambaye hana nafasi klabuni hapo. Independent.

Klabu ya Chelsea, inataka kukopa pauni milioni 500 (sh
trilioni 1.45) kwa ajili ya kujenga uwanja wao mpya ili kuepuka kutegemea fedha
za bosi wao, Roman Abramovich. Times.
Beki wa kati wa Liverpool na Ufaransa, Mamadou Sakho
(30) hajajumuishwa kwenye orodha ya wachezaji wa timu hiyo inayokwenda kwenye
ziara nchini Ujerumani. Liverpool Echo.
Kiungo wa Borussia Dortmund, Mikel Merino (21) yuko
karibu kukamilisha dili lake la uhamisho kuelekea Newcastle United ya
Uingereza. Evening Chronicle.
Tottenham inamfukuzia kiungo wa Benfica ya Ureno, Ljubomir
Fejsa (28), ili kuimarisha eneo la kati la timu hiyo. Sun.
No comments