Carrick akabidhiwa unahodha Man United huku Januzaj akipigwa bei
LOS ANGELES-
KLABU ya Manchester United imemchagua kiungo wake wa kati, Michael Carrick kuwa
nahodha wa klabu hiyo.
Carrick (35)
kwa sasa ndiye mchezaji aliyeichezea Man United kwa kipindi kirefu, baada ya
kujiunga na United 2006 na anachukua nafasi ya Wayne Rooney ambaye amehamia
klabu ya Everton.
“Nahisi ni
fursa kubwa kuiongoza uwanjani timu kama Manchester United. Sikudhani kwamba,
nitasalia katika klabu hii kwa muda huu mrefu na kufanikiwa hivi .Nimekuwa
nikiipenda klabu hii na kuwa katika nafasi hii ni kitu maalum kwangu,” Carrick
aliiambia MUTV.
Kwa upande
mwingine, klabu hiyo imekubali kumuuza mshambuliaji wao, Adnan Januzaj (22) kwa
Real Sociedad ya Hispania, kwa dau la pauni milioni 9.8 (sh bilioni 284) baada
ya mchezaji huyo kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha United.
No comments