Header Ads

Kuwaona Mayweather na McGregor ni milioni 330



https://usatmmajunkie.files.wordpress.com/2017/05/floyd-mayweather-conor-mcgregor-stances.jpg

LAS VEGAS- TIKETI za kushuhudia pambano la masumbwi kati ya Floyd Mayweather dhidi ya Conor McGregor, zinauzwa kwa dola 150,000 (sh milioni 330).
Pambano hilo ambalo linatajwa kuwa ghali kwa gharama zaidi kuwahi kutokea, lakini hilo halijawazuia wapenda masumbwi kununua tiketi kwani kwa sasa zinanunulika kama njugu.
Mabondia hao wamekuwa wakitambiana, wanataraji kuzicha mnamo Agosti 26, mwaka huu katika uwanja wa T-Mobile wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 20,000 mjini hapa.
Mayweather mwenye miaka 40, awali alistaafu lakini aliamua kurejea ulingoni tena ili kumnyamazisha McGregor ambaye ni bingwa wa ngumi za vizimba.
BBC.

No comments

Powered by Blogger.