Header Ads

Tesla yaanza kuuza magari ya umeme kwa wafanyakazi wake



https://media4.s-nbcnews.com/j/newscms/2017_30/2088441/2017-07-13t011046z_1946549674_rc1be3758c10_rtrmadp_3_usa-funds-tesla_99f4c60bd337d6b6eccc3ce04b02a7ae.nbcnews-ux-600-480.jpg

CALIFORNIA- MKURUGENZI wa kampuni ya Tesla, Elon Musk amesema ilikuwa ni vigumu kwao kutengeneza aina ya magari ya kutumia umeme ambayo yamekamilika kwa sasa.
Kauli hiyo ya Musk imekuja katika wakati ambapo baadhi ya mataifa kama Ufaransa na Uingereza, tayari yameeleza kuwa mwisho wa magari yanayotumia mafuta ni 2040.
Tayari Tesla imekamilisha magari 30, ambayo yalitolewa jana ili kuanza kuuzwa kwa wanunuzi ambao ni wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Nje ya ya jengo la Tesla katika eneo la Fremont, Musk alionesha magari hayo ambayo yatauzwa kwa dola 35,000 (sh milioni 77) yenye uwezo wa kukimbia umbali wa kilometa 350 kwa saa.
Kabla ya tukio hilo, Musk alikiri kuwa ilikuwa vigumu zaidi na iliwachukua muda na rasilimali kuweza kukamilisha utengenezaji wa magari hayo yaitwayo Model 3.
“Kwa kweli ilikuwa ni changamoto kubwa. Tunatarajia kupita katika kipindi kingine cha miezi sita migumu, ambayo ni sawa na kutengeneza kuzimu ili kukamilisha utengenezaji wa magari mengine,” alisema Musk.
NBC News

No comments

Powered by Blogger.