Header Ads

Korea Kaskazini yafanya jaribio tena



https://ichef-1.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/C2C5/production/_97116894_northkorea1.jpg

SEOUL- MOAFISA wa Serikali nchini pamoja na Japan, wamesema Korea Kaskazini imefanya jaribio jingine la kombora ambalo limeonekana likianguka katika eneo la bahari karibu na Japan.
Jaribio hilo linakuja katika kipindi ambacho, Marekani ilitoa onyo kuwa taifa hilo linaweza likafanya jaribio muda wowote na tayari imetangaza kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo vipya.
Kombora hilo lilirushwa kutoka mkoa wa Jagang, ulio Kaskazini mwa taifa hilo, kulingana na chombo cha habari Yonhap.
Katibu wa Baraza la Mawaziri nchini Japan, Yoshihide Suga alisema kuwa kombora hilo lilisafiri kwa takriban dakika 45 ikilinganishwa na kombora la masafa marefu lililofanyiwa majaribio mwanzoni mwa Julai mwaka huu.
Anasema kuwa lilianguka katika bahari ya Japan, lakini siyo katika maji ya himaya ya Japan.
Kulingana na taarifa ya Yonhap, Rais Moon Jae-in alilazimika kuitisha mkutano wa kiusalama usiku wa kuamkia leo.
Mapema Julai mwaka huu, Korea Kaskazini ilidai kufanikiwa kulifanyia jaribio kombora la masafa marefu kwa mara ya kwanza. Kombora hilo ni la hivi karibuni, katika msururu wa makombora yaliyofanyiwa majaribio hatua inayokiuka marufuku ya UN.
Umbali wa kombora hilo haujulikani licha ya kupingwa, lakini wataalam wanasema kuwa linaweza kufika Alaska nchini Marekani.
Msemaji wa Pentagon, Jeff Davis alisema kuwa kombora hilo lilirushwa na kwamba habari zaidi zinasubiriwa. Kombora hilo la hivi karibuni ni la 14 kurushwa na Korea Kaskazini kwa mwaka 2017.
BBC.



No comments

Powered by Blogger.