Asubuhi Yetu; Neymar kusaini miaka 5 PSG # Barcelona ni aidha Coutinho au Hazard # Liverpool yamsusa Keita
![https://www.thesun.co.uk/wp-content/uploads/2017/07/nintchdbpict000327391444.jpg?strip=all&w=960&quality=100](https://www.thesun.co.uk/wp-content/uploads/2017/07/nintchdbpict000327391444.jpg?strip=all&w=960&quality=100)
PARIS- MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Neymar (25)
amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano na klabu ya PSG na anatarajiwa
kujiunga na klabu hiyo wiki ijayo. RMC.
Barcelona imesema iwapo Neymar ataondoka wiki ijayo, basi italazimika
kusajili aidha, Philippe Coutinho wa Liverpool au Eden Hazard wa Chelsea ama
Dele Alli wa Tottenham Hotspurs. Hata hivyo, Barcelona wanahofia kuwa Liverpool
itawatajia bei kubwa kwa Coutinho. Mirror.
![https://www.thisisanfield.com/wp-content/uploads/PA-29223818-600x339.jpg](https://www.thisisanfield.com/wp-content/uploads/PA-29223818-600x339.jpg)
Liverpool imeachana na kwa kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita (22), baada
ya kuona timu hiyo ya Ujerumani haiku tayari kumuachia mchezaji huyo. Hata hivyo,
wamesema watajaribu kumsajili mwakani wakati thamani yake ikiwa pauni milioni
48 (sh bilioni 139). Liverpool Echo.
Manchester City wamesema watamlipa pauni milioni 320,000 wa wiki, Alexis
Sanchez (28), iwapo mchezaji huyo atajiunga nao msimu huu. Mchile mwenzake,
Claudio Bravo amesema Sanchez atapokelewa kwa mikono miwili Etihad. Mail.
![https://metrouk2.files.wordpress.com/2017/01/630734652.jpg?w=620&h=408&crop=1](https://metrouk2.files.wordpress.com/2017/01/630734652.jpg?w=620&h=408&crop=1)
Manchester United wameanza mazungumzo yenye lengo la kumsainisha mkataba
mpya kiungo wao Ander Herrera (27), ili kuzuia dili lolote kutoka Barcelona
ambao wamekuwa wakimhitaji. Express.
Kwa mujibu wa wakala wa kiungo wa Udinese ya Italia, Jakub Jankto (21), Arsenal
wameonesha kuvutiwa na dili la kumsaini kiungo huyo. Sportitalia.
![https://metrouk2.files.wordpress.com/2017/07/663328494.jpg?w=748&h=471&crop=1](https://metrouk2.files.wordpress.com/2017/07/663328494.jpg?w=748&h=471&crop=1)
Monaco bado wanasema hawatamuuza winga wao, Thomas Lemar (21) licha ya
Arsenal kuwasilisha ofa yao kwa mara ya tatu yenye thamani ya pauni milioni 45
(sh bilioni 130.5). Telegraph.
PSG imesema itamtoa winga wake mahiri, Angel di Maria (29) kwa Barcelona
ili kupunguza nyongeza zozote zinazotarajiwa kuongezeka kwenye dili la uhamisho
wa Neymar wenye thamani ya pauni milioni 197 (sh bilioni 525.5) AS.
Southampton wanahitaji kuendelea kuwa na beki wao, Virgil van Dijk (26)
na wamemuahidi kuwa kwenye kikosi cha kwanza licha ya Mdachi huyo kuachwa na
timu hiyo iliyopo ziarani Ufaransa wiki hii. Telegraph.
![https://metrouk2.files.wordpress.com/2017/05/679707230.jpg?w=748&h=552&crop=1](https://metrouk2.files.wordpress.com/2017/05/679707230.jpg?w=748&h=552&crop=1)
West Ham wamesema watakataa ofa yoyote kutoka Liverpool, yenye nia ya
kuwashawishi kuwauzia kiungo Manuel Lanzini (24). Evening Standard.
![https://metrouk2.files.wordpress.com/2017/07/gabriel1.jpg](https://metrouk2.files.wordpress.com/2017/07/gabriel1.jpg)
Kinda wa Brazil, Gabriel Martinelli (16) yuko kwenye majaribio Manchester
United wakati akitaraji kukamilisha dili la uhamisho kutoka klabu yake ya
Ituano. Manchester Evening News.
No comments