Jioni leo; Liverpool watenga £80m kwa Keita # Man Utd wamfuata Renato # Morata afuzu vipimo
LEIPZIG-
TIMU ya RB Leipzig imejikuta katika wakati mgumu wa kukataa dau la pauni milioni
80 (sh bilioni 232), ambalo limewekwa mezani na Liverpool kwa ajili ya
kumsajili, Naby Keita (22). Liverpool
Echo.
Manchester United
wamejitosa kwenye dili la kumsajili kiungo wa Bayern Munich na Ureno, Renato
Sanches (19), baada ya mchezaji huyo kushindwa kufanya vema Allianz Arena. Daily Star.
Mshambuliaji wa zamani
wa Real Madrid, Alvaro Morata (24) amefuzu vipimo vya afya na anatarajiwa
kusaini mkataba rasmi na timu hiyo, baada ya Chelsea kukubali kulipa ada ya
pauni milioni 58 (sh bilioni 168.2). Sky
Sports.
Arsenal wamepewa
nafasi ya kumsajili kiungo wa Barcelona, Rafinha kwa dau la pauni milioni 27
(sh bilioni 78.3). Wiki iliyopita, Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu
alisema mchezaji huyo anaweza akaondoka. Sky
Sports.
Stoke City
wamefanikiwa kukamilisha usajili la beki wa kati wa Chelsea, Kurt Zouma, kwa
mkopo wa mwaka mzima. Sky Sports.
Kiongozi wa akademi ya
Manchester United, Nicky Butt amesema timu hiyo itaendelea kuwapa vipaumbele
wachezaji watokanao na akademi za timu hiyo. Sky Sports.
West Ham imekamilisha
dili la kumsajili mshambuliaji wa Bayer Leverkusen ya Ujerumani, Javier
Hernandez ‘Chicharito’ na anatarajiwa kutua London muda wowote kukamilisha
vipimo vya afya na kusaini mkataba. Sky
Sports.
No comments